Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda

Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua kichwa chake kabla ya imamu wake, kuwa Mwenyezi Mungu kukifanya kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda.

فوائد الحديث

Maamuma anapokuwa na imam kuna hali nne: haliTatu zimekatazwa, nazo ni: Kumtangulia, na kwenda naye sawa, na kuchelewa, na mafundisho kwa maamuma: Ni kumfuata imam.

Ulazima wa maamuma kumfuata imam ndani ya swala.

Ahadi ya adhabu ya kubadilika sura kwa atakayenyanyua kichwa chake kabla ya imam na kuwa sura ya punda ni jambo linawezekana, nako ni kufutwa kwa sura halisi.

التصنيفات

Hukumu ya Imamu na Maamuma.