Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu

Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-: "Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hatoingia peponi ila muumini, na wala haikamiliki imani na wala haitengemai hali ya jamii ya kiislamu mpaka wapendane baina yao. Kisha akaelekeza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika jambo muhimu zaidi ambalo litaleta mapenzi kwa wote, nalo ni waislamu kutoleana salam baina yao, aliyoifanya Mwenyezi Mungu kuwa ni salam kwa waja wake.

فوائد الحديث

Kuingia peponi hakui ila kwa imani.

Katika ukamilifu wa imani ni muislamu kumpendelea muislamu mwenzake yale anayoyapenda yeye.

Ni sunna kutoa salam na kuisambaza kwa waislamu; kwa sababu kuisambaza ni kusambaza mapenzi na amani baina ya watu.

Salam haitolewi ila kwa muislamu; kwa kauli yake Rehema na amani ziwe juu yake: "Baina yenu".

Kutoa salam kunaondoa chuki na kuhamana na vifundo.

Umuhimu wa mapenzi kati ya waislamu nakuwa hilo ni katika ukamilifu wa imani.

Imekuja katika hadithi nyingine kuwa namna ya salam kamili ni: "As-salaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", na inatosha: "Assalaam alaikum".

التصنيفات

fadila za matendo ya viungo.