إعدادات العرض
Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini". Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: "Ni neno jema
Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini". Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: "Ni neno jema
Kutoka kwa Anasi Bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini". Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: "Ni neno jema".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tagalog Français ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහල Русский Svenska ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Tiếng Việt پښتو অসমীয়া دری Malagasy or Čeština नेपाली Oromoo Română Nederlands Soomaali తెలుగు Српски ไทย മലയാളം Kinyarwanda Кыргызча ಕನ್ನಡالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuambukizana ambako walikuwa wakiamini watu wa zama za ujinga kuwa maradhi yanahama yenyewe kwenda kwa mwingine pasina kadari ya Mwenyezi Mungu, nikuwa madai hayo ni batili, nakuwa mikosi ya ndege ni batili, nayo ni mikosi kupitia kitu chochote chenye kuhisika au kuonekana, kama ndege au wanyama, au walemavu, au namba au siku au kinginecho, hapa ametaja ndege kwa sababu ni kitendo kilichokuwa maarufu zama za ujinga, na asili yake ilikuwa ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi yoyote, kama safari au biashara au kinginecho, akiruka kuelekea kushoto mtu anaamini ni mkosi, na anaahirisha alichotaka kukifanya. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa anafurahishwa sana na mtu kujipa matumaini, nayo ni mtu kuwa na furaha na raha, kwa maneno mazuri anayoyasikia, yatakayomfanya awe na dhana nzuri na Mola wake Mlezi.فوائد الحديث
Kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa hakuna awezaye kuleta kheri isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna awezaye kuzia shari isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Katazo la kuamini mikosi ya ndege, nayo ni kila kitu kinachoaminika kuwa ni mkosi, na kufanya kazi isifanyike.
Matumaini si katika mikosi iliyokatazwa, bali ni katika kumdhania kheri Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kila kitu kinachotokea ni kwa mipango na makadirio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, yeye pekee asiye na mshirika wake.