Nilimpa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kusikia na kutii, na nasaha kwa kila muislamu

Imepokelewa kutoka kwa Jariri Bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimpa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kusikia na kutii, na nasaha kwa kila muislamu.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza swahaba Jariiri Bin Abdallah radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye alishikamana na maamrisho na akampa ahadi Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutekeleza swala tano za faradhi usiku na mchana, kwa kutimiza sharti zake na nguzo zake na wajibu zake na sunna zake, na kutelekeza zaka ya wajibu, nayo ni ibada ya mali ya lazima, huchukuliwa toka kwa matajiri na kupewa wanaostahiki katika mafakiri na wengineo, na kuwatii viongozi, na kumpa nasaha kila muislamu, na hii ni kwa kuchunga masilahi yake, na kumfikishia kheri, na kumkinga na shari kwa kauli na vitendo.

فوائد الحديث

Umuhimu wa swala na zaka, nazo ni katika nguzo za Uislamu.

Umuhimu wa nasaha na kunasihiana kati ya waislamu, mpaka wakampa ahadi ya utiifu Masahaba radhi za Allah ziwe juu yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

التصنيفات

Fadhila za Swala.