Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake

Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yanayomsibu muislamu katika maradhi na msongo na huzuni na misukosuko na majanga na shida mbali mbali na hofu na njaa, hata kama utakuwa ni mwiba utakaomchoma na kumuumiza, hilo kwake linakuwa ni kafara ya madhambi kwake na kifuta makosa.

فوائد الحديث

Kumebainishwa fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake waumini na huruma yake kwao kwa kuwasamehe madhambi hata kwa madhara madogo yanayowasibu.

Ni lazima kwa muislamu ataraji malipo kwa Allah kwa yale yanayomsibu, na asubiri kwa dogo na kubwa, ili iwe ni sababu ya kunyanyuliwa daraja na ni kafara ya makosa.

التصنيفات

Ubora wa Tauhiid.