Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto

Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto

Kutoka kwa Abuu Absi Abdir-Rahmani bin Jabri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Maana ya hadithi: nikuwa yule anayetoka barabarani kwaajili ya kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu -Mtukufu- ikapata vumbi miguu yake hiyo itakuwa ni sababu ya kumkinga na moto, na katika tamko la Bukhariy: "Itakayepata vumbi miguu yake katika njia ya Mwenyezi Mungu atamharamisha Mwenyezi Mungu na moto".

التصنيفات

Fadhila za Jihadi.