Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii

Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu ni mzuri na ni mtakasifu ametakasika na kila mapungufu na aibu na amesifika kwa yote yaliyokamilika, na wala hakubali katika matendo kauli na itikadi isipokuwa ile itakayokuwa nzuri, nayo ni ile iliyotakaswa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yenye kwenda sambamba na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na haitakiwi mtu ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa hayo, na katika mambo yanayosababisha amali kuwa nzuri kwa muumini ni chakula chake kuwa kizuri, na kiwe kimetokana na halali, kwa hilo amali zake zinakuwa njema, na ndio maana Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waumini kwa lile alilowaamrisha Mitume, ikiwemo kula halali na kutenda mema, akasema: "Enyi Mitume! Kuleni katika vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" Na akasema: "Enyi mlioamini kuleni katika vizuri katika vile tulivyokuruzukuni". Kisha akatahadharisha rehema na amani ziwe juu yake kula haramu,ambako kunaharibu matendo na kunazuia kukubalika kwake kwa sababu yoyote ile inayoonekana; ikiwemo: Ya kwanza: Kuwa na safari ndefu iliyo katika misingi ya kumtii Mwenyezi Mungu kama Hija na Jihadi na kuunga udugu na mengineyo. Ya pili: Nywele kukaa hovyo kwa kutotanwa, na kubadilika rangi ya ngozi na rangi ya nguo kwa sababu ya udongo, basi mtu huyu anakuwa kadharurika. Ya tatu: Ananyanyua mikono yake juu mbinguni kwa dua. Ya nne: Anamuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina yake na anang'ang'ania katika hilo: Ewe Mola wangu Ewe Mola wangu! Na pamoja na sababu hizi za kujibiwa dua hakusikilizwa; na hii ni kwa sababu chakula chake na kinywaji chake na mavazi yake ni vya haramu, na afya yake imetokana na haramu, ni mbali sana kwa mtu mwenye sifa kama hizi kujibiwa, na atajibiwa vipi?!

فوائد الحديث

Ukamilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika dhati yake, na sifa zake, na vitendo vyake, na hukumu zake.

Amri ya kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Kutumia maneno yenye kuhamasisha kufanya matendo, kiasi kwamba alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha Mitume", anapojua muumini kuwa hili ni katika yale waliyoamrishwa Mitume basi anapata nguvu na anahamasika kulitekeleza.

Katika vizuizi vya kujibiwa dua ni kula vya haramu.

Katika sababu za kujibiwa dua ni mambo matano: La kwanza: Kuwa na safari ndefu, kwakuwa ndani yake kuna kudhoofika, ambayo ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa. La pili: Wakati wa kudharurika. La tatu: kunyoosha mikono kuelekea mbinguni. La nne: Kung'ang'ania kwa Mwenyezi Mungu kwa kurudiarudia kusema ewe Mola Mlezi, na ni katika maneno makubwa ambayo hutumika kwa lengo la kutaka kujibiwa. La tano: Kula chakula kizuri na vinywaji vizuri.

Kula halali nzuri ni katika sababu zinazosaidia kutenda amali njema.

Amesema Kadhi: Kizuri ni kinyume cha kibaya, akisifiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hukusudiwa kuwa ametakasika na mapungufu, na ametukuka hana maafa, na akisifiwa mja moja kwa moja basi hukusudiwa kuwa hana tabia chafu na matendo mabaya, na anajipamba na kinyume cha hayo, na ikisifiwa mali basi hukusudiwa inapokuwa ya halali katika mali bora.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Sababu za Kujibiwa Dua.