Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utakuwa katika nafasi yake kabla hajasema neno lake alilolisema

Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utakuwa katika nafasi yake kabla hajasema neno lake alilolisema

Kutoka kwa Mikidadi bin Amri Al-Kindi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba yeye alisema kumuuliza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Unaonaje ikiwa nitakutana na mtu miongoni mwa makafiri, tukapigana, akapiga moja ya mikono yangu kwa upanga akaukata, kisha akajificha katika mti, akasema: Nimejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, je nimuue ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu baada ya kuwa amelisema neno hilo? Akasema: "Usimuue" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kakata moja ya mikono yangu, Kisha akasema hivyo baada ya kuwa kaukata?! Akasema: "Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utakuwa katika nafasi yake kabla hajasema neno lake alilolisema".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mikidadi bin Aswadi radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi atakapokutana na mtu miongoni mwa makafiri katika mapambano, wakapambana kwa mapanga, mpaka yule kafiri akakata mmoja kati ya mikono yake kwa upanga, kisha kafiri akamkimbia na akajikinga katika mti, akasema: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, je, ni halali kwangu kumuua baada yakuwa amekata mkono wangu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Hapana, usimuuwe. Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lakini yeye kakata moja ya mikono yangu, pamoja na hivyo bado tu nisimuuwe?! Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hapana, usimuuwe, kwa sababu tayari damu yake ishakuwa haramu, kwa sababu ikiwa utamuua baada ya kusilimu kwake; basi hakika yeye atakuwa katika nafasi yako ya kulindwa damu kwa Uislamu wake, na wewe utakuwa katika nafasi yake, itakuwa halali damu yako kwa kukuua kwa kisasi kwa sababu ya kumuuwa.

فوائد الحديث

Yatakayejitokeza kwake yanayoonyesha kuingia katika Uislamu kama kauli au kitendo, ni haramu kumuua.

Atakaposilimu mmoja kati ya makafiri wakati wa vita, basi damu yake itakingwa, na ni lazima kutomuua, isipokuwa tukibaini kinyume na hilo.

Ni lazima muislamu matamanio yake yafuate sheria na si mihemuko na kutaka kulipiza kisasi.

Amesema bin Hajari: Inafaa kuuliza matatizo kabla hayajatokea, kwa kuzingatia kauli sahihi kuwa kisa hiki aliuliza kabla jambo halijatokea, ama yaliyopokelewa kutoka kwa baadhi ya wema waliotangulia kulichukia hilo, hilo linatafsirika kuwa hutokea mara chache sana, ama yanayowezekana kutokea kwa kawaida ni sheria kuyaulizia ili yafahamike.

التصنيفات

Uislamu