Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi

Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi.

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Ilikuwa katika muongozo wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi na anayapokea; kwa sababu ni mepesi kubebeka na yana harufu nzuri.

فوائد الحديث

Inapendeza kukubali zawadi ya marashi; kwa sababu hakuna tabu kuyabeba kwake na wala hakuna masimango ikiwa mtu atayakubali.

Ukamilifu na tabia njema za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kutokataa marashi, na kukubali zawadi ya yeyote mwenye kumzawadia.

Himizo la kutumia marashi.

التصنيفات

Adabu za Ziara kuto asalamu na kubisha Hodi.