Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga

Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga, na atakayepigana chini ya bendera kibubusa anachukia kwa sababu ya ndugu zake, au akahamasisha katika (kupendelea kwa sababu ya) udugu, au ana nusuru udugu, akauwawa, basi hicho ni kifo cha zama za ujinga, na atakayejitoa katika umma wangu, akimpiga mwema wake na muovu wake, na wala hajali muumini wake, na wala hamtimizii mwenye ahadi ahadi yake, basi huyo si miongoni mwangu na mimi si miongoni mwake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetoka katika kuwatii viongozi, na akaeneza fitina na kuusambaratisha umoja wa Uislamu uliokubaliana juu ya kumtii kiongozi, akafa katika hali hiyo ya faraka na kutomtii kiongozi, atakuwa kafa kifo cha watu wa zama za ujinga, ambao walikuwa hawamtii kiongozi yeyote wala hawajiungi katika kundi moja, bali walikuwa makundi makundi na wabaguzi, wakipigana wao kwa wao. ... Na akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayepigana chini ya bendera ambayo haiko wazi upande wa haki au batili, anachukia kwa sababu ya ubaguzi wa watu wake au kabila lake, na si kwa kuitetea dini na haki, akapigana kwa ubaguzi pasina kuwa na ujuzi na elimu, akiuawa katika hali hiyo, atakuwa ni sawa na aliye uawa katika zama za ujinga. Nakuwa atakayetoka katika Umma wake -Rehema na amani ziwe juu yake- akimpiga mwema wake, na muovu wake, na wala hajali anayoyafanya na wala haogopi adhabu zake kwa kumuuwa muumini, na wala hawatendei uadilifu makafiri waliochukua ahadi au viongozi, bali anatengua ahadi kwao, jambo hili ni katika madhambi makubwa, atakayelifanya atakuwa amestahiki ahadi hii ya adhabu kali.

فوائد الحديث

Kuwatii viongozi ni wajibu katika mambo yasiyomuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kuna tahadhari kubwa kwa aliyetoka katika utiifu kwa kiongozi, na akasambaratisha umoja wa waislamu, akifa katika hali hii, atakuwa amekufa katika njia ya watu wajinga.

Katika hadithi kuna katazo la kupigana vita kwa sababu ya ubaguzi.

Ulazima wa kutimiza makubaliano.

Katika utiifu na kushikamana na umoja kuna heri nyingi, na amani na utulivu, na hali kutengamaa.

Katazo la kujifananisha na watu zama za ujinga.

Amri ya kushikamana na umoja wa waislamu.

التصنيفات

Kutoka kwa ajili ya kumpinga kiongozi.