kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera

kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera

kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- "kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera"

[Sahihi]

الشرح

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kila kinachoondosha akili na kuiondoa hicho ni pombe yenye kulewesha, sawa iwe ni kunywa, au kula, au kuvuta kwa pumzi au vinginevyo, na kuwa kila kinacholevya na kuondoa akili Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiharamisha na amekataza, kiwe kidogo au kingi, Na kuwa kila mwenye kunywa aina yoyote ya vileo, na akaendelea kuvinywa, wala hakutubia mpaka akafa; Anastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kumnyima kuinywa Peponi.

فوائد الحديث

Sababu ya kuharamishwa pombe ni kilevi, hivyo, kila chenye kulevya kiwe kwa aina yoyote ile ni haramu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha pombe; kwakuwa imekusanya madhara na maovu makubwa.

Kunywa pombe peponi ni katika ukamilifu wa ladha na utimilifu wa neema.

Ambaye hakuizuia nafsi yake na unywaji pombe duniani Mwenyezi Mungu atamharamishia kuinywa peponi, kwani malipo huendana na matendo.

Hili ni himizo la kufanya haraka kutubia dhidi ya madhambi kabla ya kifo.

التصنيفات

Vinywaji na vilivyoharamishwa.