Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu

Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alingia kwangu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikiwa nimeweka pazia lenye picha kwa kusahau, alipoliona akalichana na akaghadhibika mpaka uso wake ukabadilika rangi, na akasema: "Ewe Aisha, Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu" Aisha anasema: "Tukalichana vipande vipande vingine tukavifanya kuwa mto au mito miwili ya kulalia".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia nyumbani kwake kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake akamkuta akiwa kafunika ghala dogo ambalo huhifadhiwa humo bidhaa kwa kitambaa ambacho kina picha za viumbe hai, ikabadilika rangi ya uso wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa hasira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akalifunua, na akasema: Watu wenye adhabu kali zaidi siku ya Kiyama ni wale wenye kufanya mfano kwa kutengeneza picha za vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu. Aisha akasema: Tukakifanya kitambaa kile kuwa ni mto mmoja au miwili.

فوائد الحديث

Kukemea uovu wakati wa kuuona na kutochelewa katika hilo, madam hakuna madhara makubwa katika hilo.

Adhabu siku ya Kiyama itatofautiana kulingana na ukubwa wa dhambi.

Kupiga picha za viumbe hai ni katika madhambi makubwa.

Miongoni mwa hekima za kuharamishwa kupiga picha za viumbe hai ni kufafanisha vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu, sawa sawa mpigaji awe kakusudia kufananisha au hakukusudia hivyo.

Sheria imetilia umuhimu juu ya kuhifadhi mali kwa kuitumia katika matumizi mengine baada ya kuitoa katika matumizi ya haram.

Katazo la kutengeneza picha za viumbe hai kwa umbile lolote lile litakalokuwa, hata kama litakuwa ni dhalili.

التصنيفات

Kumpwekesha Allah kwa vitendo vyake(Uumbaji)