Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima

Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amru -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe unafunga milele, na unasimama usiku?", Nikasema: Ndiyo, akasema: "Hakika wewe ukifanya hivyo macho yatadhoofu, na nafsi itanyongeka, Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima", Nikasema: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hapo, akasema: "Basi funga swaumu Daudi amani iwe juu yake, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na wala hakimbii anapokutana (na adui)".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ilimfikia habari Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akiunganisha swaumu na wala hafungui mwaka mzima, na anaswali usiku mzima wala halali, akamkataza hilo na akamwambia: Funga na ufungue, na simama na ulale. Na akamkataza kuunganisha swaumu na kusimama usiku mzima, na akamwambia: Hakika wewe ukifanya hivyo macho yako yatadhoofika na yatabonyea, na itanyong'onyea kwa hilo nafsi yako na itachoka nakuwa na unyonge; hana swaumu atakayefunga mwaka mzima; kiasi ambacho hakupata malipo ya swaumu kwa kwenda kinyume na katazo, na hakufungua kwa sababu aliendelea. Kisha akamuelekeza kufunga siku tatu katika kila mwezi, hizo ni sawa na swaumu ya mwaka mzima; kwa sababu kila siku moja ni sawa na siku kumi, ambayo ndiyo ziada ndogo zaidi ya mema. Akasema Abdullah: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hizo. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Basi funga swaumu ya Daudi amani iwe juu yake na ndiyo swaumu bora, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na alikuwa hakimbii anapokutana na adui; kwa sababu namna ya swaumu yake haikudhoofisha mwili wake.

فوائد الحديث

Kufunga siku tatu katika kila mwezi ni kama kufunga mwaka mzima, na hii ni kwa sababu jema moja hulipwa mara kumi mfano wake, zinakuwa siku thelathini, akifunga katika kila mwezi siku tatu anakuwa kana kwamba kafunga mwaka mzima.

Miongoni mwa njia za ufikishaji ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni kuhamasisha katika amali na kueleza thawabu zake na thawabu za kudumu na amali hiyo

Amesema Khattwabi: Muhutasari wa kisa cha Abdallah bin Amri nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hajamuwekea ibada ya swaumu pekee mja wake, bali kamuwekea aina mbali mbali za ibada, hata angemaliza juhudi zake zote angepunguza katika ibada zingine, jambo bora ni kuwa kati na kati ili abakishe baadhi ya nguvu kwa ajili ya ibada zingine, na limeashiriwa hilo katika kauli yake rehema na amani ziwe juu yake kwa Daudi amani iwe juu yake: "Na alikuwa hakimbii anapokutana na adui"; kwa sababu alikuwa akipata nguvu kwa kufungua kwa ajili ya Jihadi.

Katazo la kuzama na kujikalifisha katika ibada, na kheri inakuwa kwa kushikamana na sunna.

kauli ya jopo la wanachuoni ni kuchukiza kufunga milele, na inakuwa ni haramu atakapoipa tabu nafsi na akaidhuru, na akaibebesha mzigo mzito, na akaachana na sunna ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake, na akaitakidi kuwa isiyokuwa sunna yake ndiyo bora kuliko sunna.

التصنيفات

Funga za Kujikurubisha.