Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana

Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana

Kutoka kwa Barraa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana".

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hakuna waislamu wawili watakaokutana njiani na mfano wake wakasalimiana kwa kupeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana kwa viwiliwili au kwa kumaliza kupeana mikono.

فوائد الحديث

Sunna ya kupeana mikono wakati wa kukutana, na himizo juu yake.

Amesema Manawi: Na sunna haipatikani isipokuwa kwa kuweka mkono wa kulia katika mkono wa kulia kiasi kwamba hakuna udhuru.

Himizo la kusambaza salamu, na kumebainishwa ukubwa wa malipo ya kumpa mkono muislamu ndugu yake muislamu.

Kunavuliwa katika hadithi kupeana mikono kwa haramu, kama kumpa mkono mwanamke wa kando.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema., Adabu za kuto asalamu na kubisha Hodi.