Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake

Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake

Imepokelewa kutoka kwa Othman bi Affan -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetawadha kwa kuchunga sunna za udhu na adabu zake, hilo litakuwa katika sababu za kusamehewa makosa na kufuta madhambi, "Mpaka yatoke" madhambi yake kutoka chini ya kucha za mikono yake na miguu yake.

فوائد الحديث

Himizo la kutilia umuhimu wa kujifunza udhu na sunna zake na adabu zake, na kuzifanyia kazi.

Ubora wa udhu, nakuwa hilo ni kafara ya madhambi madogo, ama makubwa ni lazima kufanya toba.

Sharti za kutoka kwa madhambi ni kuukamilisha udhu na kuuleta bila mapungufu kama alivyobainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Kufutwa kwa madhambi katika hadithi hii kumefungamanishwa na kuyaepuka madhambi makubwa na kuyaombea toba, amesema Mtukufu: "Ikiwa mtayaepuka madhambi makubwa mnayokatazwa tutakusameheni makosa yenu" [An-Nisaa: 31].

التصنيفات

Fadhila - ubora wa kutawadha.