إعدادات العرض
kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo
kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu: kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo, na ama kunipinga kwake ni kauli yake: Mwenyezi Mungu hatonirudisha kuwa hai, kama alivyonianzisha, na si kuanza kuumba ni kwepesi zaidi kwangu kuliko kurudisha, na kunitukana kwake ni kauli yake: kuwa Mwenyezi Mungu kajifanyia mwana, na mimi ndiye mmoja mwenye kukusudiwa, sikuzaa wala sikuzaliwa, na wala hakuna anayefanana nami hata mmoja".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල Svenska ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە Tiếng Việt پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or Malagasy Čeština नेपाली Oromoo Română Nederlands Soomaali తెలుగు ไทย മലയാളം Српски Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Lietuvių Wolof Magyar ქართული Mooreالشرح
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil Qudsi yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameeleza kuhusu washirikina na makafiri kuwa wao humkanusha na humsifu kwa sifa za mapungufu na za aibu, na hawakutakiwa kufanya hivyo. Ama kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu: Ni kudai kwao kuwa Mwenyezi Mungu hatowarejesha kwa mara nyingine baada ya kufa kwao kama alivyowaumba mara ya kwanza kutoka katika kutokuwepo, akawajibu kuwa aliyeanza kuumba mwanzo anauwezo wa kuwarudisha, bali hilo ni jepesi mno, japo kuwa uhalisia kwa Mwenyezi Mungu yote ni mepesi, kuumba kwanzia mwanzo na kurudisha, kwani Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza. Na ama kutukana kwao: Ni kauli yao: Kuwa yeye ana mtoto, akawajibu kuwa yeye ni wa pekee aliyepwekeka kwa ukamilifu wote katika majina yake na sifa zake na vitendo vyake, aliyetakasika na kila mapungufu na aibu, wa pekee asiyehitaji kwa yeyote, na anahitaji kwake kila mmoja, na hakuwahi kuwa mzazi wa yeyote, na hakuwahi kuwa mtoto wa yeyote, na hakuna yeyote anayefanana naye hata mmoja kwa kuwa na mfanano au mwendano, ametakasika na kutukuka.فوائد الحديث
Kuthibitisha ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu.
Kumethibitishwa kufufuliwa baada ya kifo.
Kukufuru mwenye kupinga kufufuliwa au akamnasibishia mtoto Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu hana mfano wala mwenye kufanana naye.
Upana wa upole wa Mwenyezi Mungu, na kuwapa kwake muda makafiri huenda wakatubia na kurejea.