Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe

Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe

Kutoka kwa Ally amesema: Hakika mimi nilikuwa ni mtu kila nikisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hadithi Mwenyezi Mungu ananinufaisha kwa hadithi hiyo kwa kiasi alichotaka kuninufaisha, na akinihadithia yeyote katika Masahaba zake ninamuapisha, akiniapia ninamuamini, na siku moja alinihadithia Abubakari, na Abubakari akasema ukweli, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe", Kisha akasoma aya hii: "Na wale ambao wakifanya machafu au wakizidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakaomba msamaha kutokana na madhambi yao" [Al-Imran: 135].

[Sahihi]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna mja yeyote atakayetenda dhambi, akatawadha vizuri, kisha akasimama na akaswali rakaa mbili kwa nia ya kuomba toba kutokana na dhambi lake hili, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasoma kauli yake Mtukufu: "Na wale ambao wakitenda dhambi kubwa au wakizidhulumu nafsi zao kwa kutenda dhambi chini ya hizo, wanaikumbuka ahadi ya Mwenyezi Mungu ya malipo mema kwa wanaomtii na malipo mabaya kwa wanaomuasi na wanaelekea kwa Mola wao hali ya kutubia wakawa wanamuomba Awasamehe madhambi yao na wakawa wana yakini kwamba hapana anayesamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wao kwa sababu hiyo hawaendelei kwenye maasi, na wao wanajua kwamba wakitubia Mwenyezi Mungu Atawakubalia toba yao". [Surat Al-Imran: 135].

فوائد الحديث

Himizo la kuswali kisha kuomba msamaha baada ya kutenda dhambi.

Upana wa msamaha wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kukubali kwake toba na msamaha.

التصنيفات

Toba