إعدادات العرض
Atakayesema: Laa ilaah illa llaah, na akayapinga yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu itakuwa haramu mali yake na damu yake, na hesabu yake itakuwa juu ya Allah
Atakayesema: Laa ilaah illa llaah, na akayapinga yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu itakuwa haramu mali yake na damu yake, na hesabu yake itakuwa juu ya Allah
Kutoka kwa Twariki bin Ashiyam Al-Ashjai Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesema: Laa ilaah illa llaah, na akayapinga yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu itakuwa haramu mali yake na damu yake, na hesabu yake itakuwa juu ya Allah".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ ไทย Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە සිංහල دری Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Română Kinyarwanda नेपाली Српски Wolof Soomaali Moore Українська Българскиالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema na akashuhudia kwa ulimi wake yakuwa "Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu", Yaani: Hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na akayakanusha yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na akajitenga na dini zote isipokuwa Uislamu, itakuwa haramu mali yake na damu yake kwa muislamu, hatumiliki isipokuwa dhahiri katika matendo yake, hapokonywi mali yake na wala haimwagwi damu yake, isipokuwa atakapofanya uhalifu au jinai linalopelekea hivyo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu. Na Allah atasimamia hesabu yake siku ya Kiyama, akiwa ni mkweli atamlipa, na akiwa mnafiki atamuadhibu.فوائد الحديث
Kutamka Laa ilaaha illah llaah, na kuyapinga yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, ni sharti la kuingia katika Uislamu.
Maana ya (Laa ilaaha illa llaah) ni kupinga kila kinachoabudiwa kinyume na Allah yakiwamo masanamu na makaburi na mengineyo, na kumpwekesha yeye Mtukufu kwa ibada.
Atakayeileta tauhidi na akashikamana na sheria zake kwa dhahiri ni wajibu kujizuia kutomtendea baya mpaka yabainike yanayokwenda kinyume na hilo.
Uharamu wa kula mali ya Muislamu na kumwaga damu yake na kuvunja heshima yake ila kwa haki.
Hukumu duniani ni kwa yale yanayoonekana, na akhera ni katika nia na makusudio.