Basi tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ilikuwa ni Qur'ani

Basi tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ilikuwa ni Qur'ani

Amesema Sa'd bin Hisham bin Aamiri -alipoingia kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake: Ewe mama wa waumini, nieleze kuhusu tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akasema: Hivi si unasoma Qur'ani? Nikasema: Ndiyo! akasema: Basi tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ilikuwa ni Qur'ani.

[Sahihi]

الشرح

Aliulizwa mama wa waumini Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuhusu tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akajibu kwa neno lilokusanya, na akamuhamisha muulizaji upande wa Qura''ani tukufu iliyo kusanya sifa za ukamilifu, kama alivyosema -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiiga tabia za Qur'ani, iliyoyaamrisha Qur'ani anayaamrisha, na yale inayoyakataza Qur'ani anayaepuka, basi ikawa tabia yake ni kuifanyia kazi Qur'ani, na kusimama katika mipaka yake na kua na adabu na adabu zake kuizingatia Qur'ani na matendo kwa ujumla na mfano wake.

فوائد الحديث

Himizo la kumuiga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika kujipamba kwake na tabia za Qur'ani.

Kusifiwa kwa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, nakuwa tabia hizo zilikuwa zikitoka katika taa ya wahyi.

Qur'ani ndio chimbuko la kila tabia njema.

Tabia katika Uislamu zinakusanya dini yote, kwa kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo.

التصنيفات

Sifa za kitabia.