“Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio

“Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio, atasema: Nilikutakeni jambo jepesi zaidi kuliko hili, nanyi mkiwa katika mgongo wa Adam: yakuwa msinishirikishe na chochote, mkakataa isipokuwa kunishirikisha na chochote".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu ambao watateswa kidogo na Moto wa Jahannam baada ya kuingia humo: Lau mngekuwa na dunia na vyote vilivyomo ndani yake, mngeweza kujikomboa kutokana na mateso haya? Watasema: Ndio, Basi Mwenyezi Mungu atasema: Nilikutaka na nikakuamrisheni jambo jepesi kuliko hilo, ilipo chukuliwa ahadi kwenu mkiwa katika mgongo wa Adam, ya kwamba msinishirikishe na chochote. Nilipowatoa katika dunia hii mlikataa kufanya chochote isipokuwa ushirikina.

فوائد الحديث

Thamani ya tauhidi na wepesi wa kuifanyia kazi.

Hatari ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu kingine na mwisho wake mbaya.

Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kwa wanadam wote wakiwa katika mgongo wa baba yao Adam ya kutomshirikisha.

Tahadhari ya ushirikina nakuwa thamani ya dunia yote haiwezi kumsaidia chochote kafiri siku ya Kiyama.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.