Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha

Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha"

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy - Imepokelewa na Imamu Muslim - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa rehema hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha za viumbe hai; Hii ni kwa sababu sura ya kitu ambacho kina roho ni dhambi kubwa, na kuna uigaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na ni njia katika njia za ushirikina, na baadhi yake ni picha ya vile vinavyoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu. Ama sababu ya kujiepusha na nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa; ni kwa sababu anakula uchafu mwingi, na ni kwa sababu baadhi mbwa huitwa mashetani; Na malaika wako dhidi ya mashetani. Na kwa sababu ya harufu mbaya ya mbwa; Malaika wanachukia harufu mbaya, na kwa sababu ni haramu kuwafuga; Hivyo mwenye kuwafuga akaadhibiwa kwa kunyimwa Malaika kuingia nyumbani kwake, na kuswali humo, na kumuombea msamaha, kumbariki yeye na nyumba yake, na kumzuilia udhia wa Shetani.

فوائد الحديث

Uharamu wa kufuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au mifugo au mazao.

Kuwa na picha ni miongoni mwa mambo maovu ambayo Malaika huchukizwa nayo, na kuwepo kwake mahali hapo ni sababu ya kunyimwa huruma, na hivyo hivyo kwa mbwa.

Malaika ambao hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha ni Malaika wa rehema, lakini kwa walinzi na wengine ambao wana kazi kama Malaika wa mauti, wanaingia kila nyumba.

Uharamu wa kutundika picha za viumbe wenye roho juu ya kuta na kwingineko.

Amesema Al-Khattwabi: Bali Malaika hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha, jambo linalopelekea uharamu wa kumiliki mbwa na picha, ama mbwa wasiokuwa haramu ni kama vile mbwa wa kuwinda, wa mazao, na wa mifugo, na picha zinazotumika katika zulia, mito, na vitu vingine, kwa kukanyagwa na kudhalilishwa hizi haziwezi kuwa sababu ya kuzuia Malaika kuingia.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.