إعدادات العرض
Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku
Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, husema: "Ni nani anayeniomba nimjibu? Ni nani anayenitaka shida yake nimpe? Ni nani anayeniomba msamaha nimsamehe?".
[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tagalog Kurdî Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் සිංහල မြန်မာ ไทย Русский 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە Hausa دری Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Română Kinyarwanda नेपाली Српски Soomaali Deutsch Moore Українська Български Wolof Azərbaycan ქართული тоҷикӣالشرح
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka huteremka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, na anawahamasisha waja wake wamuombe, kwani yeye anamjibu mwenye kumuomba, na anawahimiza wamtake haja zao, kwani yeye humpa anayemuomba, na anawaita wamuombe msamaha kutokana na madhambi yao kwani yeye huwasamehe waja wake waumini.فوائد الحديث
Ubora wa theluthi ya mwisho ya usiku na swala na dua na kutaka msamaha ndani yake.
Ni wajibu kwa mwanadamu wakati wa kusikia hadithi hii awe na pupa kubwa ya kunufaika na nyakati za kujibiwa dua.