Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia

Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mama Salama alimsimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kisa cha kanisa aliloliona katika ardhi ya Ethiopia, likiitwa kanisa la Mtakatifu Maria, akasimulia aliyoyaona ndani yake miongoni mwa picha, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia, na wanachora ndani yake picha hizo, hao ndio viumbe waovu zaidi mbele ya Allah

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amesimulia mama wa waumini mama Salama radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba alipokuwa katika ardhi ya Ethiopia aliona Kanisa -linaloitwa kwa jina la Mtakatifu Maria- ndani yake kukiwa na picha na mapambo na michoro; akastaajabu kwa kitendo hicho!. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akafafanua sababu za kuwekwa picha hizo; Akasema: Hakika hao unaowataja hapa walikuwa anapokufa kwao mtu mwema wanajenga Msikiti juu ya kaburi lake, na wanasali ndani yake, na wanachoro picha hizo, Na akabainisha kuwa mfanyaji wa hilo ni kiumbe muovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu kitendo chake hicho kinapelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

فوائد الحديث

Uharamu wa kujenga Misikiti juu ya makaburi, au kuswali hapo, au kuzika maiti ndani ya msikiti; hii ikiwa ni kuziba njia za kuelekea katika ushirikina.

Kujenga Misikiti juu ya makaburi, na kutundika picha, hiki ni kitendo cha Mayahudi, nakuwa mwenye kufanya hivi atakuwa kafanana nao.

Uharamu wa kutengeneza picha za viumbe hai (wenye roho).

Atakayejenga msikiti juu ya kaburi na akachoro ndani yake picha, huyu ni katika viumbe waovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Sheria imeuhami sana upande wa tauhidi kwa himaya iliyokamilika, kwa kuziba njia zote ambazo zinaweza kusababisha kufika katika ushirikina.

Katazo la kuchupa mipaka kwa watu wema; kwani ni sababu ya kuingia katika shirki.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake., Hukumu za Misikiti.