Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo

Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika adabu za wajibu kwa atakayehudhuria hotuba ya Ijumaa: Ni kunyamaza na kumsikiliza hatibu; ili mtu azingatie mawaidha, nakuwa atakayezungumza walau kwa jambo dogo, na imamu akihutubu, akasema kumwambia mwenzie: "Nyamaza" na "Sikiliza", basi zitakuwa zimempita fadhila za swala ya Ijumaa.

فوائد الحديث

Uharamu wa mazungumzo wakati wa hotuba, hata kama ni kuzia uovu au kujibu salamu au kumuombea dua aliyepiga chafya.

Anaondolewa katika katazo hili atayemsemesha imamu au imamu akamsemesha yeye.

Inafaa kuzungumza kati ya hotuba mbili.

Akitajwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na imamu akiwa katika hotuba basi unatakiwa kumswalia kwa siri, na hivyo hivyo kuitikia dua.

التصنيفات

Swala ya Ijumaa