Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani

Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba mtu wa kijijini alimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani" Akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha zaidi ya hapo, basi alipoondoka, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayependezwa na kumtazama mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame huyu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alikuja mtu mmoja miongoni mwa watu wa vijijini kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili amjulishe kuhusu amali itakayomuingiza peponi, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kuwa kuingia peponi na kuokoka na moto yote haya yanasimama katika nguzo za Uislamu, kuanzia kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na usimshirikishe na kitu chochote katika ibada. Na usimamishe swala tano alizoziwajibisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake katika kila usiku na mchana. Na utoe zaka ya mali aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu juu yako, na uitoe kuwapa wastahiki wake. Na uhifadhi na kudumu nayo swaumu ya ramadhani katika wakati wake. Yule bwana akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha chochote zaidi ya amali hizo za faradhi nilizozisikia toka kwako katika ibada, na wala sitopunza chochote katika hizo. Alipoondoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Yeyote atakayependezwa na kumuangalia mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame bedui (Mtu wa kijijini) huyu.

فوائد الحديث

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ibada ndio jambo la kwanza ambalo huanzwa nalo katika kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu.

Kutosheka na mafunzo ya wajibu pekee kwa mgeni katika Uislamu.

Kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu lazima kuanza ngazi kwa ngazi.

Pupa ya mtu kujifunza swala la dini yake.

Muislamu akitosheka na ibada za wajibu pekee basi atafaulu, lakini hii haimaanishi kufanya uzembe katika ibada; kwa sababu sunna hukamilisha mapungufu ya faradhi.

Kuzitaja baadhi ya ibada pasina zingine, ni dalili ya umuhimu wake na himizo juu ya ibada hizo, na haimaanishi kuwa hakuna zingine zaidi yake.

التصنيفات

Adabu za mjuzi na mwenyekujifunza.