Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa

Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa".

[قال النووي: حديث حسن] [رواه ابن ماجه والبيهقي وغيرهما]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wake katika hali tatu: La kwanza: Kukosea, nayo ni yale yanayotokea kwao pasina kukusudia, nayo ni muislamu kukusudia kufanya jambo lolote, kisha kitendo chake kikakutana na jambo ambalo hakulikusudia. La pili: Kusahau, nako ni muislamu kuwa na kumbukumbu ya kitu, lakini akakisahau wakati wa kufanya, hana madhambi katika hilo pia. La tatu: Kulazimishwa, mja anaweza kulazimishwa kufanya kitu ambacho hakitaki pamoja na kutoweza kuzuia kulazimishwa, na hapo pia hatopata dhambi au ubaya. Pamoja na tahadhari kuwa maudhui ya hadithi ni katika yale yalio baina ya mja na Mola wake katika kufanya maharamisho, ama kuacha maamrisho kwa kusahau hapa haiondoki, na ama kitendo chake kikiambatana na kosa la jinai hii pia haiondoki katika haki ya kiumbe, kama akiua kimakosa, atatakiwa kutoa fidia, au akaharibu gari kwa makosa atawajibika kulipa.

فوائد الحديث

Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upole wake kwa waja wake kiasi ambacho amewaondolea madhambi pale yatakapojitokeza maasi katika hali hizi tatu.

Fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya umma wake.

Kuondolewa dhambi haimaanishi kuondolewa hukumu au dhamana, mfano atakayesahau udhu, na akaswali kwa kudhani kuwa yuko twahara, hana dhambi katika hilo, lakini atatakiwa kutia udhu na kurudia swala.

Lazima katika kuondolewa dhambi kwa kulazimishwa kuwe na sharti, mfano kama akiwa mlazimishaji anauwezo wa kutimiza alichotishia.

التصنيفات

Kumuamini Allah mwenye nguvu alie tukuka