Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia

Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia

Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (basi malipo yake yatakuwa) ni kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya kuipata dunia, au kwa ajili ya mwanamke atakaemuoa, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kile alichokiendea." Na lafudhi ya Bukhari: ""Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na miamala, atakaye kusudia kupata masilahi katika amali yake hatopata zaidi ya masilahi na wala hatopata thawabu, na atakayekusudia katika amali yake kujiweka karibu na Allah Mtukufu, atapata thawabu na malipo kupitia amali yake hata kama litakuwa ni jambo la kawaida, kama kula na kunywa. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.

فوائد الحديث

Himizo la kuwa na Ikhlasi (kutakasa nia) kwani Mwenyezi Mungu hakubali katika matendo isipokuwa yale yatakayokusudiwa kupata radhi zake.

Matendo ambayo hutumika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwayo, akiyafanya muislamu mtu mzima kwa njia ya mazoea hawezi kuwa na thawabu juu yake, mpaka akusudie kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo hayo.

التصنيفات

Matendo ya moyoni.