Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpaka adhikike

Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpaka adhikike

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpaka adhikike".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anakataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwaanza Mayahudi na Wakristo kwa salam, hata kama watakuwa wamepewa hifadhi katika nchi za kiislamu, achilia mbali makafiri wengineo, na akabainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tutakapokutana na mmoja wao njiani tumbane mahala pembamba, muumini ndiye atembee katikati ya njia, na anayepisha ni kafiri, na muislamu asiwe dhalili kwa hali yoyote ile.

فوائد الحديث

Haitakiwi kwa muislamu kumuanza yeyote katika Mayahudi na Wakristo kwa salam, na makafiri wengineo.

Inafaa kujibu salam zao wao watakapoanza kutoa salam kwa kusema: Na kwenu pia.

Haitakiwi kwa muislamu kukusudia kumuudhi kafiri kwa kumbana kwa makusudi pasina sababu; ili amsukumie mahala pafinyu pa njia; lakini njia ikiwa nyembamba au inamsongamano basi muislamu ndiye mwenye haki zaidi, na kafiri ndiye apishe.

Kudhihirisha utukufu wa waislamu na unyonge wa wasiokuwa wao, pasina kuwadhulumu au kuwaambia maneno machafu.

Kuwabana makafiri ni kwa sababu ya ukafiri walionao wa kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, huenda hilo likawa sababu ya kusilimu; akasalimika na moto, ikiwa hilo litawafanya kujua sababu ya kufanyiwa hivyo.

Hakuna ubaya kwa muislamu kumwambia kafiri mwanzo wa mazungumzo, vipi hali yako?, Umeamkaje? Umeshindaje? Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo; kwa sababu katazo hapa linachukuliwa ni katika salam ya kiislamu.

Amesema Attwayibi: Kauli iliyopendekezwa nikuwa mtu wa bida haanzwi kwa salam, na akimsalimia asiyemjua kisha akabaini kuwa si muislamu asema: Nimerudisha salam yangu, kama kumdharau.

التصنيفات

Adabu za kuto asalamu na kubisha Hodi.