Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake

Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake

Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akautazama mwezi usiku (yaani: Usiku wa tarehe 15) akasema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake, ikiwa mtaweza kufanya hima msizidiwe mkashindwa kusali kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo" Kisha akasoma: "Na umtukuze Mola wako kwa himdi zake njema kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Walikuwa Masahaba pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika usiku mmoja akatazama katika mwezi (Usiku wa terehe kumi na nne (14), akasema: Hakika waumini wote watamuona Mola wao Mlezi kwa hakika kabisa kwa macho bila kutatizika, nakuwa hawatosukumana na wala hawatopata tabu wala uzito wakati wa kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ikiwa mtaweza kuzizuia sababu ambazo zinakuzuieni kuto swali swala ya Alfajiri na swala ya Alasiri basi fanyeni hivyo, na zitekelezini kikamilifu ndani ya wakati wake na katika jamaa, kwani hilo ni miongoni mwa sababu za kuuona uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasoma -Rehema na amani ziwe juu yake- Aya "Na utakase sifa za Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake"

فوائد الحديث

Habari njema kwa watu wa imani ya kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu peponi.

Katika njia za kufikisha ujumbe ni: Kusisitiza na kuhamasisha na kupiga mifano.

التصنيفات

Maisha ya Akhera.