Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)

Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)

Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".

[Sahihi]

الشرح

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwanamke haikubaliki ndoa yake ila kwa walii atakayesimamia kufungwa kwa ndoa.

فوائد الحديث

Walii ni sharti la kusihi ndoa, ikifanyika bila walii, au mwanamke akajiozesha mwenyewe, haikubaliki.

Walii ni ndugu wa karibu wa kiume kwa mwanamke, asiozeshwe na walii wa mbali akiwepo walii wa karibu yake.

Ni sharti kwa walii: Awe mtu mzima (Aliyebalehe), mwanaume, na uwezo wa kupambanua na kujua masilahi ya ndoa, na wawe katika dini moja, msimamizi na msimamiwa, asiyekuwa na sifa hizi hastahiki kuwa msimamizi wa kufungisha ndoa.

التصنيفات

Ndoa.