إعدادات العرض
Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu
Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu
Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema: Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".
[Sahihi]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල Svenska ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە Tiếng Việt پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or Malagasy नेपाली Čeština Oromoo Română Nederlands Soomaali తెలుగు ไทย മലയാളം Српски Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Lietuvių Wolof ქართული Magyar Moore Українськаالشرح
Anaeleza swahaba mtukufu Abdullah Bin Khubaib radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa wao walitoka katika usiku wenye mvua kubwa, na giza lilikuwa nene, kwa ajili ya kumtafuta Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake; ili awasalishe, wakamkuta, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Sema" Yaani: Soma, akawa hakusoma kitu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akarejea kauli yake kwake, Abdullah akasema: Nisome nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Soma suratul Ikhlaswi (Qul-huwallaahu ahadi), na sura mbili za kinga (Qul-Audhubirabbil-falaq), na (Qul-Audhubirabbin-naas), wakati wa jioni, na wakati wa asubuhi, mara tatu tatu, zitakuhifadhi na kila shari, na zitakukinga na kila baya.فوائد الحديث
Sunna ya kusoma Suratul Ikhlasi na sura mbili za kinga asubuhi na jioni, nakuwa sura hizo ni kinga dhidi ya kila shari.
Ubora wa kusoma suratul Ikhlasi na sura mbili za kinga.
التصنيفات
Nyiradi za Asubuhi na Jioni.