إعدادات العرض
Hakika Imani huoza na kudhoofika kwenye mwili wa mmoja wenu kama inavyooza nguo mpya kwa kukaa muda mrefu, basi muombeni Mwenyezi Mungu aifanye Imani kuwa mpya kwenye nyoyo zenu
Hakika Imani huoza na kudhoofika kwenye mwili wa mmoja wenu kama inavyooza nguo mpya kwa kukaa muda mrefu, basi muombeni Mwenyezi Mungu aifanye Imani kuwa mpya kwenye nyoyo zenu
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Umar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Imani huoza na kudhoofika kwenye mwili wa mmoja wenu kama inavyooza nguo mpya kwa kukaa muda mrefu, basi muombeni Mwenyezi Mungu aifanye Imani kuwa mpya kwenye nyoyo zenu."
[Sahihi] [Imepokelewa na Al Haakim]
الترجمة
عربي English မြန်မာ Svenska cs ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Español Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe Bosanski සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa മലയാളം తెలుగు ไทย پښتو অসমীয়া Shqip دری el bg ff it kn Кыргызча Lietuvių mg or ro Русский rw Soomaali Српски тоҷикӣ uz नेपाली mosالشرح
Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Imani huoza katika moyo wa muislamu na inachakaa kama inavyochakaa nguo mpya kwa kutumika muda mrefu; Na kuoza huko ni kwa sababu ya udhaifu katika ibada, au kwa sababu ya kufanya maasi na kuzama kwenye matamanio. Basi anatoa muongozo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tumuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu azifanye kuwa mpya imani zetu, kwa kutekeleza mambo ya wajibu na kuzidisha kumtaja Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha.فوائد الحديث
Himizo la kumuomba Mwenyezi Mungu uimara na kuzifanya kuwa mpya imani katika nyoyo.
Imani sahihi ni kauli matendo na itikadi, na imani inazidi kwa kutii, na hupungua kwa kufanya maasi.
التصنيفات
Kuzidi kwa Imani na Kupungua kwake.