Kwa hakika miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondolewa elimu, na kuzidi ujinga, na kukithiri uzinifu, unywaji pombe, na wanaume watakuwa wachache na wanawake watakuwa wengi mpaka itafikia wanawake hamsini kusimamiwa na mwanaume mmoja

Kwa hakika miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondolewa elimu, na kuzidi ujinga, na kukithiri uzinifu, unywaji pombe, na wanaume watakuwa wachache na wanawake watakuwa wengi mpaka itafikia wanawake hamsini kusimamiwa na mwanaume mmoja

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nitawahadithieni Hadithi nimeisikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-, na hadithi hiyo hatowahadithia yeyote asiyekuwa mimi: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake anasema: "Kwa hakika miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondolewa elimu, na kuzidi ujinga, na kukithiri uzinifu, unywaji pombe, na wanaume watakuwa wachache na wanawake watakuwa wengi mpaka itafikia wanawake hamsini kusimamiwa na mwanaume mmoja."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika alama za kukaribia Kiyama ni kuondolewa elimu ya sheria na kuondolewa kwake itakuwa ni kwa kufa wanachuoni. Na matokeo yake utazidi na utaenea ujinga, na uzinifu utaenea na uchafu, na unywaji pombe utazidi na idadi ya wanaume itapungua na ya wanawake itazidi; Mpaka itafikia hatua mwanaume mmoja atabeba mambo yao na kusimamia maslahi yao.

فوائد الحديث

Kumewekwa wazi baadhi ya alama za Kiyama.

Kujua muda wa Kiyama ni katika mambo ya ghaibu (yasiyoonekana wala kujulikana) ni katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaficha.

Himizo juu ya kujifunza elimu ya kisheria kabla ya kukosekana kwake.

التصنيفات

Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa), Ubora wa Elimu.