Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni

Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni

Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemsemea uongo kwa makusudi kwa kumnasibishia kauli au kitendo kwa uongo, basi atambue kuwa Akhera atakua na makazi motoni; ndio malipo yake kwa kumsingizia kwake uongo.

فوائد الحديث

Kumsemea uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa makusudi kabisa ni sababu ya kuingia motoni.

Kumsemea uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- si sawa na kuwasemea uongo watu wengine, kwa kuwa hilo linaambatana na madhara makubwa katika dini na dunia.

Hii ni tahadhari ya kusambaza hadithi kabla ya kuthibitisha usahihi wake kuwa ni kweli zimenasibishwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- au la!.

التصنيفات

Umuhimu wa sunnah naNafasi yake., Tabia mbovu.