إعدادات العرض
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitaja jambo fulani, akasema: "Jambo lenye kuogopesha litakuwa wakati itakapo ondoka elimu
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitaja jambo fulani, akasema: "Jambo lenye kuogopesha litakuwa wakati itakapo ondoka elimu
Imepokelewa kutoka kwa Ziyaad Bin Labiid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitaja jambo fulani, akasema: "Jambo lenye kuogopesha litakuwa wakati itakapo ondoka elimu" Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni vipi inaondoka elimu, na hali yakuwa sisi tunaisoma Qur'ani na tunawasomesha watoto wetu na watoto wetu wanawasomesha watoto wao mpaka siku ya Kiyama? Akasema: "Akukose mama yako ewe Ziadi ikiwa nitakuzingatia wewe ni miongoni mwa wajuzi katika mji wa Madina, hivi hawa siyo Mayahudi na Manaswara wanaisoma Taurati na Injili, na hawafanyii kazi chochote katika yale yaliyomo?!"
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Español Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe Bosanski සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa മലയാളം తెలుగు ไทย پښتو অসমীয়া Shqip دری Ελληνικά Български Fulfulde Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Română Kinyarwanda Српски тоҷикӣ O‘zbek नेपाली Moore Kurdî Wolof Soomaali Français Oromoo Azərbaycan Tagalog Українська mr தமிழ் bm Deutsch ქართული Português Македонски Magyar Lingala Русский 中文الشرح
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amekaa kati ya Maswahaba zake, akasema: Huu ndiyo wakati ambao itaondolewa na kupokonywa elimu kutoka kwa watu, Hivyo akashangaa Ziyaad Bin Labiid Al-Answaariy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Akasema: Ni vipi itaondolewa elimu na kutupotea sisi?! Na hali yakuwa tumeisoma Qur'ani na tukaihifadhi; Namuapia Mwenyezi Mungu kuwa tutaisoma, na kuwasomesha wake zetu na watoto wetu, na wajukuu wetu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa anaona ajabu: Amekukosa mama yako ewe Ziyaad! kama ikiwa nitakuzingatia wewe ni katika wajuzi wa mji wa Madina! Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akaweka wazi kuwa kuiokosa elimu siyo kuikosa Qur'ani, bali kukosa elimu ni kuacha kuifanyia kazi, Kwa mfano hii hapa Taurati na Injili ipo kwa Mayahudi na Manaswara; na pamoja na hivyo haiwanufaishi, wala hawapati faida kutokana na makusudio yake; na faida yenyewe ni kufanyia kazi walicho jifunza.فوائد الحديث
Kuwepo kwa Misahafu na vitabu kwenye mikono ya watu, haviwafai pasina kuvifanyia kazi.
Kuondoshwa elimu kunakuwa kwa mambo mengi, miongoni mwayo ni: Kufariki kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kufa kwa Maulamaa, na kuacha kuifanyia kazi elimu.
Miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondoka elimu na kuacha kuifanyia kazi.
Kuhimizwa kuifanyia kazi elimu, na hayo ndiyo makusudio.
التصنيفات
Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa)