Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikua akisema mwishoni mwa kila swala ya faradhi

Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikua akisema mwishoni mwa kila swala ya faradhi

Kutoka kwa Warraadi mwandishi wa Mughira amesema: Alinisomea Mughira bin Shu'ba katika kitabu kilichoandikwa kwenda kwa Muawia: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikua akisema mwishoni mwa kila swala ya faradhi: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul mulku walahul hamdu, wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Allaahumma laa maania limaa a'twaita walaa mu'twiya limaa mana'ta, walaa yanfa'u dhal jaddi minkal jaddu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kabla kidogo ya mwisho wa kila swala ya faradhi: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul mulku walahul hamdu, wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Allaahumma laa maania limaa a'twaita walaa mu'twiya limaa mana'ta, walaa yanfa'u dhal jaddi minkal jaddu" Yaani: Nina kiri na kulikubali neno la kumpwekesha Allah, la Laa ilaaha illa llaah, -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah-, ibada ya kweli naithibitisha kwa Mwenyezi Mungu, na ninaikanusha kwa asiyekuwa yeye, hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allah, na ninakiri kuwa ufalme wa kweli uliotimia ni wa Mwenyezi Mungu, na sifa zote za viumbe wa mbinguni na ardhini zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, kiasi kwamba yeye ndiye muweza juu ya kila kitu, na aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu katika vipawa au kunyimwa hakuna awezaye kuyazuia, na hapo basi utajiri hauwezi kumsaidia mwenye nao, bali kinachoweza kumfaa ni amali zake.

فوائد الحديث

Kupendeza kusomwa dua hii mwisho wa swala kwakuwa imekusanya lafudhi za tauhidi na himdi.

Kufanya haraka kuitekeleza sunna, na kuitangaza.

التصنيفات

Adh-kaar - yasomwayo- wakati wa swala.