إعدادات العرض
Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu
Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu".
الترجمة
العربية Tagalog Português دری অসমীয়া বাংলা Kurdî پښتو Hausa Tiếng Việt Македонски O‘zbek ភាសាខ្មែរ ਪੰਜਾਬੀ Moore తెలుగు اردو Azərbaycan ไทย አማርኛ Magyar Türkçe ქართული 中文 ಕನ್ನಡ ગુજરાતી Українська Shqip हिन्दी Кыргызча Српски Kinyarwanda тоҷикӣ Wolof Čeština Русский Bahasa Indonesia English தமிழ் नेपाली മലയാളം kmr فارسی Bambara ms Bosanski Lietuviųالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kuwa miongoni mwa mazuri ya ukamilifu wa Uislamu wa Muislamu na ukamilifu wa imani yake, ni kujiweka kwake mbali na yale yasiyomuhusu na yale yasiyo na faida kwake miongoni mwa kauli na matendo, au katika yale yasiyomuhusu miongoni mwa mambo ya dini na dunia, mtu kushughulika na yale yasiyomuhusu huenda likamshughulisha akaacha yale yanayomuhusu, au likampelekea katika yale yanayomlazimu kuyaepuka; kwani mwanadamu ataulizwa kuhusu matendo yake siku ya Kiyama.فوائد الحديث
Watu wanatofautiana katika Uislamu wao, na kwamba Uislamu huzidi uzuri kwa baadhi ya matendo.
Kuacha upuuzi na mambo yasiyo na faida miongoni mwa maneno na matendo ni dalili ya ukamili wa Uislamu wa mtu.
Himizo la mtu kushughulika na yale yanayomuhusu katika mambo ya dini yake na dunia yake, ikiwa miongoni mwa uzuri wa Uislamu wa mtu ni kuacha yale yasiyomuhusu, basi katika uzuri wake pia ni kushughulika na yale yanayomuhusu.
Amesema bin Qayyim Mwenyezi Mungu amrehemu: Na amekusanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake unyenyekevu wote katika neno moja, akasema: "Katika uzuri wa Uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu", hii inakusanya kuacha yale yasiyomuhusu: Miongoni mwa maneno na kutazama, na kusikiliza, na kushika, na kutembea, na kufikiria, na harakati zote za wazi na za siri, neno hili linatosheleza sana katika unyenyekevu.
Amesema bin Rajab: Hadithi hii ni msingi miongoni mwa misingi ya adabu.
Himizo la kutafuta elimu; kwa sababu kupitia elimu mwanadamu anajua yanayomuhusu na yasiyomuhusu.
Kuamrisha mema na kukataza maovu na kutoa nasaha ni miongoni mwa mambo yanayomuhusu mwanadamu; kwa sababu ameamrishwa kufanya hivyo.
Inaingia katika ujumla wa maana ya hadithi: Kujiweka mbali na yale yasiyomuhusu, yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka na yale aliyoyachukia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na vile vile yale asiyoyahitajia miongoni mwa mambo ya Akhera kama uhalisia wa ghaibu na ufafanuzi wa hukumu ya kuumbwa na amri, na miongoni mwake ni kuuliza na kutafuta kuhusu mambo ya kukadiria na kuchukulia, hali yakuwa bado hayajatokea, au pengine hayawezi kutokea kabisa, au hayapo kabisa.
التصنيفات
Tabia mbovu.