Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea

Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Marthad Al-Anawiy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Amekataza -Rehema na amani ziwe juu yake- kukaa juu ya makaburi. Kama alivyokataza kusali kwa kuyaelekea makaburi, kwa kaburi kuwa upande wa kibla cha mwenye kusali; kwa sababu hilo ni katika njia za shirki.

فوائد الحديث

Katazo la kusali makaburini au kati kati yake au kuyaelekea, isipokuwa swala ya jeneza kama ilivyothibiti katika mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Katazo la kusali kwa kuyaelekea makaburi ni kuziba mianya ya kuingia katika ushirikina.

Uislamu umekataa kuchupa mipaka katika makaburi na kuyadhalilisha pia, hakuna kuyapuuza wala kuyatukuza.

Heshima ya muislamu inabakia hata baada ya kufa kwake, kwa kauli yake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kuvunja mfupa wa maiti ni kama kuuvunja akiwa hai".

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake., Masharti ya Swala.