إعدادات العرض
Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu
Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Allah- rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Português සිංහල دری অসমীয়া ไทย Tiếng Việt አማርኛ Svenska Yorùbá Кыргызча Hausa ગુજરાતી नेपाली Oromoo മലയാളം Română Nederlands Soomaali پښتو తెలుగు Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Malagasy Српски Moore ქართულიالشرح
Alieleza Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aina za matumizi, na akazipanga pale panapokuwa na namna nyingi za kutoa matumizi kulingana na kile ambacho ni wajibu zaidi kwako, hivyo alianza na muhimu zaidi na kisha muhimu zaidi. Akaeleza kuwa mali yenye malipo mengi ni ile anayoitoa muislamu kwa wale anaolazimika kuwahudumia; kwanzia mkewe na watoto, kisha kutoa katika kipando kilichoandaliwa kwa ajili vita katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha kuwahudumia jamaa zake na rafiki zake wanapokuwa Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.فوائد الحديث
Mpangilio wa matumizi katika ubora ni kwa namna ulivyotajwa, lizingatiwe hilo panapokuwa na majukumu mengi.
Kumebainishwa umuhimu wa kuanza na familia katika kutoa matumizi, na ndiko kuna fadhila nyingi kuliko kutoa sehemu zingine.
Kuhudumia Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni katika kutoa kukubwa, kama kuandaa vifaa na watu kwa ajili ya Jihadi.
Inasemekana kuwa: Makusudio ya njia ya Mwenyezi Mungu ni kila jambo la ibada, mfano kama Hija.