Atakapoona mmoja wenu ndoto anayoipenda, basi hiyo imetoka kwa Mwenyezi Mungu, na amshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, na aisimulie

Atakapoona mmoja wenu ndoto anayoipenda, basi hiyo imetoka kwa Mwenyezi Mungu, na amshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, na aisimulie

Kutoka kwa Abuu Saidi Al khudriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Atakapoona mmoja wenu ndoto anayoipenda, basi hiyo imetoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na amshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, na aisimulie- Na katika riwaya nyingine: asimsimulie yeyote ila yule anayempenda- Na akiota kinyume na hivyo miongoni mwa yale anayoyachukia, basi hayo yametokana na shetani, aombe kinga kutokana na shari yake, na asiyaeleze kwa yeyote; kwani hayo hayatoweza kumdhuru".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Atakapoona muislamu usingizini mwake yale yenye kumfurahisha, basi hiyo ni habari njema toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi na amshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka kwa bishara hii njema, na asimsimulie yeyote isipokuwa yule anayempenda miongoni mwa familia yake au jirani zake au jamaa zake wale wema miongoni mwao, na akiota kinyume na hivyo miongoni mwa ndoto mbaya anazozichukia mandhari yake, au hapendi kujua ufafanuzi wake, basi hayo ni maigizo ya kishetani anayaleta shetani katika nafsi ya aliyelala usingizini mwake, ili amuhofishe na amuhuzunishe, basi akiona hivyo aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake.

التصنيفات

Adabu ya kuona Ndoto