Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe

Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa sharti za kusihi swala: Ni twahara, ni wajibu kwa atakayetaka kuswali atawadhe ikiwa kimetokea kwake kitenguzi cha udhu; kama haja kubwa au ndogo au usingizi au kinginecho.

فوائد الحديث

Swala ya mtu mwenye hadathi (kama janaba, hedhi au nifasi) haikubaliki mpaka ajitwaharishe kwa kuoga kutokana na hadathi kubwa, na kwa kutawadha ikiwa ni hadathi ndogo (kama kwenda haja kubwa au ndogo, au kulala, au kutokwa upepo)

Udhu ni kuchukua maji na kuyazungusha mdomoni na kuyatoa, kisha kuvuta maji kwa pumzi mpaka ndani ya pua, kisha kuyatoa na kuyapenga, kisha mtu ataosha uso wake mara tatu, kisha ataosha mikono yake pamoja viwiko viwili mara tatu, kisha atafuta kichwa chake mara moja, kisha kuosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu.

التصنيفات

Udhu - kutawadha., Udhu - kutawadha.