إعدادات العرض
1- Yeyote atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili, na asiizungumzishe ndani ya nafsi yake atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.
2- Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe.
3- Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, yatatoka madhambi yake mwilini mwake
4- Twahara (usafi) ni sehemu ya imani
5- Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke puani mwake maji, kisha apenge, na atakayestanji kwa mawe basi ayafanye kuwa witiri, na atakapoamka mmoja wenu toka usingizini mwake basi na aoshe mikono yake kabla hajaiingiza katika chombo mara tatu, kwani hakika mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake
6- Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu
7- Nilimshuhudia Amru bin Abii Hasan alimuuliza Abdullah bin Zaidi kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha kwaajili yao udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake
8- Adhabu kali ya moto itazipata nyayo za miguu
9- Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anapiga katika kila fundo: Unatakiwa kulala usiku mrefu basi lala
10- Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali
11- Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali
12- Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala
13- Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja
14- Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili
15- Atakapo hisi mmoja wenu chochote tumboni kwake, akapata wasi wasi, je kuna chochote kimemtoka au la?, basi asitoke msikitini mpaka asikie sauti, au anuse harufu