Atakapo hisi mmoja wenu chochote tumboni kwake, akapata wasi wasi, je kuna chochote kimemtoka au la?, basi asitoke msikitini mpaka asikie sauti, au anuse harufu

Atakapo hisi mmoja wenu chochote tumboni kwake, akapata wasi wasi, je kuna chochote kimemtoka au la?, basi asitoke msikitini mpaka asikie sauti, au anuse harufu

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapo hisi mmoja wenu chochote tumboni kwake, akapata wasi wasi, je kuna chochote kimemtoka au la?, basi asitoke msikitini mpaka asikie sauti, au anuse harufu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kitakapotatiza chochote tumboni kwa mwenye kusali, akapata shaka, je kuna chochote kimemtoka au la?, asiondoke katika swala yake na akaikatisha kwa ajili ya kurudia udhu, mpaka apate uhakika wa kutenguka udhu wake; ima kwa kusikia sauti ya upepo, au anuse harufu; kwa sababu mwenye uhakika habatilishi uhakika wake kwa shaka, hali yakuwa ana uhakika na twahara, na hadathi (kutengukwa udhu) kunatiliwa shaka.

فوائد الحديث

Hadithi hii ni msingi katika misingi ya Uislamu, na ni kanuni miongoni mwa kanuni za kisheria, nayo ni; Yakini haiondoki kwa shaka, na asili ni kubaki hali iliyokuwa kama ilivyokuwa, mpaka mtu apate uhakika wa kinyume chake.

Shaka haiathiri katika twahara, na mswaliji ataendelea kubaki katika twahara yake madama hajapata uhakika wa hadathi (kutengukwa udhu).

التصنيفات

Fomula za Kifq'hi na za Kiusulu., Vyenye kuharibu Udhu.