Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo

Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo

Imepokelewa Kutoka kwa Ibn Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Pepo na Moto viko karibu mno na mwanadamu kama ukaribu wa mwendo wa kiatu unaokuwa juu ya kisigino, kwa sababu anaweza kufanya twa'a (ibada) katika yale yanayomridhisha Allah Mtukufu akaingia Peponi kwa ibada hiyo, au dhambi moja likawa sababu ya kuingia motoni.

فوائد الحديث

Himizo la kufanya heri hata kama ni ndogo, na tishio la kufanya shari hata kama ni ndogo.

Ni lazima muislamu katika maisha yake kukusanya kati ya kutaraji mazuri na kuogopa adhabu, na kumuomba Allah Mtukufu muda wote kuthubutu (Kudumu) katika haki mpaka asalimike na wala asihadaike na hali aliyonayo.

التصنيفات

Sifa za pepo na moto.