Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi

Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi, na hakika miongoni mwa kutangaza machafu, ni mtu kutenda dhambi usiku, kisha akaamka akiwa kasitiriwa na Mwenyezi Mungu juu ya dhambi hilo, akaanza kusema: We fulani, jana usiku mimi nilifanya kadhaa wa kadhaa, hali yakuwa alilala usiku kucha Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka asubuhi anafunua pazia la Mwenyezi Mungu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu mtenda dhambi anatarajiwa kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu, isipokuwa mwenye kutangaza maasi kwa kutaka ufahari na jeuri, huyu hastahiki msamaha; anafanya maasi mchana, kisha anaamka hali yakuwa Mwenyezi Mungu kamsitiri, anaanza kumsimulia mwingine kuwa yeye jana alifanya maasi fulani, na hali yakuwa alilala Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka anafunua pazia la Mwenyezi Mungu juu yake!!.

فوائد الحديث

Ubaya wa kuweka wazi maasi baada ya kusitiriwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Katika kutangaza maasi ni kusambaza machafu baina ya waumini.

Mwenye kusitiriwa na Mwenyezi Mungu duniani atamsitiri pia Akhera, na hii ni katika upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake.

Atakayepata mtihani wa maasi, anatakiwa ajifiche, na atubie kwa Mwenyezi Mungu.

Ukubwa wa dhambi la kutangaza madhambi kwa wale wanaokusudia kuweka wazi maasi, na wanajikosesha wao wenyewe kusamehewa.

التصنيفات

Kuyasema vibaya Maasi.