Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi

Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika adabu za kutoleana salamu kati ya waislamu "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh". Mdogo amsalimie mkubwa, na aliyepanda amsalimie anayetembea kwa miguu, na anayetembea kwa mguu amsalimie aliyekaa, na idadi ndogo wawasalimie idadi kubwa.

فوائد الحديث

Sunna ya kutoa salamu kwa mujibu wa yaliyokuja katika hadithi, mtembea kwa miguu anapomsalimia aliyepanda kipando, na wengineo katika hao waliotajwa, inafaa, lakini ni kwenda kinyume na kilicho bora zaidi.

Kutoa salamu kwa namna iliyokuja katika hadithi ni katika sababu za mapenzi na kujenga umoja.

Wakiwa wanalingana na wako sawa katika hayo yaliyotajwa, basi mbora wao ni yule atakayeanza kwa salamu.

Ukamilifu wa sheria hii katika kubainisha yote anayoyahitaji mwanadam.

Kufundisha adabu za salamu na kumpa kila mwenye haki haki yake.

التصنيفات

Adabu za kuto asalamu na kubisha Hodi.