إعدادات العرض
Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja
Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja."
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහල دری অসমীয়া پښتو O‘zbek Tiếng Việt Македонски ភាសាខ្មែរ ਪੰਜਾਬੀ తెలుగు ไทย Moore አማርኛ Magyar Azərbaycan ქართული ಕನ್ನಡ ગુજરાતી Українська Shqip Кыргызча Kinyarwanda Српски тоҷикӣ Wolof Čeština தமிழ் नेपाली മലയാളം kmr msالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa inakuwa haramu kwa kunyonya sawa na uharamu wa kuzaliwa na wa nasaba kama mjomba au baba mdogo au kaka n.k. na kunyonya kuna halalisha yale yanayohalalishwa na kuzaliwa miongoni mwa hukumu.فوائد الحديث
Hadithi ni kanuni katika hukumu za kunyonya.
Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja" Yaani: Na kuna halalisha yale yanayohalalishwa, nayo kwa ujumla ni katika yale yanayohusiana na kuharamisha ndoa na yale yanayofuata, na kuenea kwa uharamu baina mnyonyaji na watoto wa mnyonyeshaji, na kuwaweka nafasi ya ndugu wa karibu katika kufaa kuwatazama na kukaa nao faragha na kusafiri pamoja, lakini hukumu zingine za umama hazihusiani na hili kama akurithiana na uwajibu wa matumizi na kuacha huru kwa umiliki na ushahidi na akili na kuondosha kisasi.
Kuthibiti kwa hukumu ya uharamu kwa kunyonya uharamu wa milele.
Hadithi zingine zimeonyesha kuwa uharamu wa kunyonya unathibiti kwa minyonyo mitano inayoeleweka, na iwe ndani ya miaka miwili ya mwanzoni.
Walioharamishwa kwa nasaba ni: Akina mama, na wanaingia hapo mabibi na kwenda juu wa upande wa mama au baba. Na mabinti: Na wanaingia humo mabinti wa mtoto wa kike, na mabinti wa mtoto wa kiume, na kwenda chini. Na madada: Sawa sawa wawe wa upande wa baba au mama, au wa upande wa mmoja wao. Na Shangazi wote: Na wanaingia hapo madada wote wa baba wa tumbo moja na wasiokuwa wa tumbo moja, na vile vile ndugu wote wa kike wa babu zako, na kwenda juu. Na Mama wadogo au wakubwa: Na wanaingia humo dada wote wa tumbo moja na mama na wengineo, na vile vile dada wote wa mabibi, na kwenda juu, sawa sawa mabibi wawe wa upande wa baba au wa mama. Na mabinti wa kaka na mabinti wa dada, na wanaingia humo mabinti zao na kwenda chini.
Wanaoharamishwa kwa sababu ya kunyonya: Wanakuwa haramu kwa kunyonya wale wanaokuwa haramu kwa nasaba, kila mwanamke aliyeharamishwa kwa nasaba mfano wake anakuwa haramu kwa kunyonya isipokuwa mama wa kaka yake na dada wa mwanaye katika kunyonya, hawa si haramu.
التصنيفات
Kunyonyesha.