Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba

Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba

imepokewa Kutoka kwa Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba".

[Sahihi]

الشرح

Anatuhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa na kuzuia madhara katika mambo ya Dunia na Akhera, kwani hakuna yeyote mwenye kutoa wala kunyima wala kudhuru wala kunufaisha isipokuwa Yeye Aliyetakasika na Kutukuka, Na tufanye sababu zinazoleta manufaa na kuzuia madhara, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa dhati, wakati wowote tutakapofanya hivyo, Mwenyezi Mungu ataturuzuku kama anavyowaruzuku ndege wanaotoka asubuhi wakiwa na njaa, kisha wanarudi jioni matumbo yakiwa yamejaa, na kitendo hiki kwa ndege ni aina ya kufanya sababu za kutafuta riziki, bila kubweteka wala uvivu.

فوائد الحديث

Ubora wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, nakuwa ni katika sababu kubwa ambazo huvuta riziki.

Kumtegemea Mwenyezi Mungu hakupingani na kufanya sababu, kwani kaeleza kuwa kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa uhakika hakupingani na kutoka asubuhi na kurudi jioni katika kutafuta riziki.

Sheria kutilia umuhimu matendo ya moyo; kwa sababu kutegemea ni katika matendo ya moyo.

Kutegemea sababu pekee ni mapungufu katika dini, na kuacha kufanya sababu ni mapungufu ya akili.

التصنيفات

Fadhila za matendo ya moyoni.