Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?

Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?" Wakasema: Hautobakiza uchafu wowote, akasema: " Huu ndio mfano wa swala tano, Mwenyezi Mungu hufuta makosa kwa swala hizo".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Amefananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- swala tano za kila usiku na mchana katika kuondoa kwake na kufuta kwake madhambi madogo ni sawa na Mto ulioko mlangoni kwa mtu akioga humo kila siku mara tano, hautobakiza chochote katika uchafu wake.

فوائد الحديث

Fadhila hizi ni maalum kwa kufuta madhambi madogo, ama makubwa hayo ni lazima kuwe na toba.

Fadhila za kutekeleza swala tano na kuzihifadhi kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake na sunna zake.

التصنيفات

Fadhila za Swala.