Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi

Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi

Kutoka kwa Amri Bin Shuab kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa baba awaamrishe watoto wake wa kiume na wa kike kusali na umri wao ukiwa mikaa saba, na awafundishe wanayoyahitaji kwa ajili ya kuitekeleza. Na wakifikisha miaka kumi azidi kutilia mkazo, awapige wanapofanya uzembe, na awatenganishe katika vitanda.

فوائد الحديث

Kuwafundisha dini watoto wadogo kabla hawajabalehe, na hasa hasa swala.

Kipigo kinakuwa ni kwa ajili kutia adabu, nasi kwa kuadhibu, apige kipigo kinachoendana na hali yake.

Sheria imetilia umuhimu kuhifadhi heshima, na kuziba kila njia inayopelekea kuiharibu.

التصنيفات

Wajibu wa Swala na Hukumu ya Mwenye kuiwacha.